Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Thomas Ulimwengu atambulishwa Singida Fountain

Klabu ya Singida Fountain Gate FC imemtambulisha mshambuliaji tishio wa Tanzania, Thomas Ulimwengu, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akicheza soka nje ya Tanzania.

Tangu kuondoka Moro United akiwa kijana mdogo mwaka 2010, hakucheza tena soka katika vilabu vya Tanzania hadi sasa aliporejea nchini na kujiunga na Singida Fountain Gate FC.

Aliitumikia TP Mazembe kuanzia mwaka 2011 Hadi 2016, akahamia AFC Eskilstuna mwaka 2017, akatimkia Sloboda Tuzle msimu wa 2017-18, kabla ya kujiunga na Al Hilal mwaka 2018, Kisha JS Saoura mwaka 2019, kabla ya kurejea tena TP Mazembe kuanzia mwaka 2020 Hadi sasa ametua Singida Fountain Gate FC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *