THBUB KUCHUNGUZA MALALAMIKO 150 YA UVUNJWAJI HAKI ZA BINADAMU

Na Gideon Gregory – Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Juma Homera amesema katika kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa na Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), itafanya uchunguzi wa malalamiko 150 (Mapya 100 na ya zamani 50) yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.

Dkt. Homera ameyasema hayo leo Aprili 24,2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2026/27 na kuongeza kuwa itafuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa katika malalamiko 25 yaliyofanyiwa uchunguzi.

Aidha, Dkt. Homera amesema THBUB itaimarisha na kuhamasisha elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora katika mikoa 20ya Tanzania bara na Zanzibar, kurusha vipindi 130 vya redio na runinga, kuanzisha klabu za haki za binadamu katika shule za Msingi, Sekondari na vyuo.

Amesema, “THBUB itafanya ukaguzi wa magereza 78, vituo 37 vya polisi, shule za maadilisho moja (1) na mahabusu ya watoto moja (1) na maeneo mengine wanamozuiliwa watu katika Mikoa 20.”

Ameongeza kuwa, Tume itafungua kesi tano (5) za uvunjwaji wa  haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *