Thabiti Kandoro C.E.O mpya Tabora United

Aliyekuwa Mkurugenzi wa mashindano wa Yanga SC, Thabiti Kandoro, ametangazwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa wegeni wa ligi Tabora United FC ya mkaoni Tabora.

Kandoro ambaye msimu uliopita alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Fountain Gate Sports ya jijini Dodoma, pamoja na mambo mengine anasifika zaidi katika kusimamia weledi, utawala Bora, kuongeza mapato kwenye timu na kutengeneza mifumo thabiti ya timu kujiendesha ipasavyo.

Akizungumza Kuhusu klabu hiyo kutokamilisha usajili kwenye mfumo wa FIFA Connect, Kandoro amesema kufikia kesho kila kitu kitakuwa tayari.

Zaidi kuhusu mipango yake kwenye timu hiyo, sikiliza THE KICK OFF kuanzia saa 19:00 Hadi 21:00 usiku wa leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *