Na William Bundala, Kahama – Shinyanga.
Rais wa chama cha mpira nchini Tanzania Wallece Karia Ameishauri halmashauri ya manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, kupitia mpango wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu kukaa na wataalamu ili kujenga uwanja wa kisasa ili uweze kutumika kwa mashindano mbalimbali ikiwemo ligi kuu ya hapa Nchini.
Karia Ametoa wito huo mjini Kahama katika ukumbi wa mikutano wa manispaa alipokutana na wadau wamichezo hususani mpira wa miguu kwaajili ya kujadili mipango ya kuinua na kukuza mpira wa miguu mkoani Shinyanga na kuongeza wigo wa ajira kwa vijana na fulsa za kibiashara.

“Kuhusu ujenzi wa uwanja niwashauri shirikianeni na wataalamu ili kuweza kujenga uwanja wa kisasa ambao utaweza kutumika kwa michezo mbalimbali ikiwemo ligi kuu ya Tanzania” Amesema Karia.
Katika hatua nyingine Karia amesema Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Iko tayari kushirikiana na wadau wa soka kuanzisha kituo cha michezo ndani ya manispaa ya Kahama kitakachowezesha vijana kuinua na kukuza kipaji ikiwa ni pamoja na kufundisha walimu wa timu za mipira na masuala yote yakimichezo.

“Hili suala la ujenzi wa kituo cha michezo halina mjadala,TFF iko tayari kushirikiana na wadau wa soka Kuanzisha kituo cha michezo ndani ya manispaa ya Kahama,kituo hiki kitasaidia kupata watoto wenye vipaji Pamoja na walimu wa kuwafundisha,pia kutakuwa na masomo ya kingereza na masomo ya Tehama ili kuwasaidia Kwenda na kasi ya dunia ilivyo” Amesongeza Karia.
Azan Mufti ni mjumbe wa TFF Kutoka Kahama Amesema katika kuunga jitihada za chama hicho ngazi ya taifa atalipia wanamichezo wanao taka kujiunga na mafunzo ya ualimu wa mpira wa miguu, yanayotarajiwa kuanza mwezi Aprili mwaka huu.

“Tunaishukuru sana TFF kwa kuliona hili kwakweli kituo hiki kitatusaidia sana,na mimi katika kuunga mkono nitalipia gharama za walimu wote watakaokuwa tayari kupata mafunzo hayo” Amesema Mufti.
Kwa upande wao Baadhi ya wadau wa mchezo huo wilayani humo Akiwemo Diwani wa kata ya majengo Mh Shida Soko Wameomba ujenzi wa uwanja huo uendane mpango wa kupata timu ya ligi kuu kwakupandisha ama kununua timu wakiitaja kahama kuwa watu wake ni wapenda soka.

“Tunakushukuru sana Rais kufika Kahama,Kahama tunapenda mpira sana na tunaomba basi ujenzi wa uwanja utusaidie tupate timu ya ligi kuu iwe kwa kuipandisha ama kununua mana Kahama tunapenda Mpira sana” Amesema Mh Soko na Ramadhani Saidi.
Manispaa ya kahama imeanza maandalizi ya ujenzi wa uwanja chenye uwezo wa kuingiza idadi ya watu wasiopungua 7000 ikiwa ni mpango wa kuongeza ajira na na mzunguko wa shughuli za kibiashara kupitia mashindano yatakayokuwa yakifanyika kupitia uwanja huo.