Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limelaani tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Padre Charles Kitima na kutoa wito kwa Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama kuchukua hatua za haraka za kuwabaini na kuwakamata waliohusika katika kupanga na kutekeleza uhalifu huo.

TEC pia imetaka uchunguzi wa tukio hilo ufanyike kwa haraka na taarifa zilitolewe kwa uwazi na bila upotoshwaji, ili kurudisha imani na matumaini kwa watu huku ikiwashukuru wote waliomsaidia na kumfikisha Padre Kitima Hospitalini mapema.
