Tazama Utalii wa ndani unaofanywa na watanzania kwenye hifadhi ya taifa kisiwa cha Rubondo

Utalii wa ndani unaofanywa na baadhi ya watanzania kwenye maeneo ya vivutio na hifadhi za Taifa ikiwemo hifadhi ya taifa kisiwa cha Rubondo iliyoko Mkoani Geita, kwa kiasi kikubwa umechangia kukua kwa uchumi na kuongeza pato la Taifa huku watanzania wakiaswa kujenga utaamaduni wa kutembelea vivutio hivyo.

Akizungumza leo na Wanahabari kutoka Mkoani Shinyanga, Alord Mwasuluka Kaimu Mkuu wa Hifadhi Rubondo amesema utalii unaofanywa kisiwani hapo unasaidia kupeleka huduma kwa jamii (CSR) kwenye vijiji jirani kupitia sekta ya afya,elimu na nyinginezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *