TAWA YAHAMASISHA WANANCHI KUTEMBELEA NA KUTUNZA VIVUTIO KIREJESHI

Na Saada Almasi – Simiyu.

Katika kuendelea kukabiliana na matukio ya ujangili unaofanywa na wananchi katika pori la akiba la Kijereshi Wilayani Busega Mkoani Simiyu, uongozi wa Pori hilo umefanya matembezi maalum na kushirikisha wakazi wa maeneo hayo ili wajionee vivutio vinavyopatikana maeneo hayo sambamba na wawahamasisha umuhimu wa kuvitunza

Akizungumza na wakazi hao muda mfupi baada ya matembezi hayo kamanda daraja la kwanza wa pori hilo Mohammed Mpita amesema kuwa kila mwananchi anatakiwa kujipa jukumu la kutunza wanyama hao kwa faida yao na vizazi vijavyo

“Jukumu la kutunza hawa wanyama si letu askari peke yetu bali la kwenu pia,tunapoacha kuwaua tunawapa maisha ambayo yatakuja kuwafaidisha watoto wetu hapo baadae” amesema Mpita.

Mpita ameongeza kuwa kwa sasa tayari mwekezaji amepatikana atakayekuja kujenga hoteli ya kitalii katika pori hilo uwekezaji ambao utawanufaisha pia wakazi wa maeneo hayo

” tumeshasaini mkataba na huyu mwekekazi atakuja hapa na kujenga hoteli ya kitalii,hii itatoa fursa hata kwenu kwa maana ya ajira mtatumika tu sasa mkiendelea kufanya uharibifu hapa hasara itawakuta pia” ameongeza Mpita 

Tumaini Patrick ni mkazi wa Bunda ambaye ametumia fursa hiyo kujifunza mambo mengi kuhusu utalii wa pori na kusema kuwa uwoga aliokuwa nao kuhusu gharama za kufika hapo sasa umekwisha.

“Mwanzo nilikuwa na hofu nikiamini kutalii katika hifadhi ni gharama kubwa lakini nimefika nimejionea uumbaji wa Mungu na niko tayari kwenda kuhamasisha wenzangu ili tuwe na utaratibu wa kufika maeneo haya na kukatazana kuwaua wanyama wetu” amesema Tumaini

Pori la akiba la Kijereshi limepakana na hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika upande wa Mashariki na Kaskazini na upande wa Magharibi na Kusini likipakana na vijiji vitano vinavyopatikana katika wilaya ya Bariadi na Busega

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *