Klabu ya soka ya Yangasc imetozwa faini ya Tsh milioni moja kwa kosa la mashabiki wake watatu (3) kuonekana kwenye eneo la vyumba vya kuvalia kuelekea mchezo wake dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa Yanga kushinda 2-1 katika dimba la Sokoine.

Pia Mchezaji Kibwana Shomari wa klabu ya Yanga ametozwa faini ya Tsh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kuonekana akiondoa taulo la mlinda mlango wa klabu ya Mashujaa lililokuwa limewekwa pembeni ya lango wakati mchezo ukiendelea, jambo lililoashiria imani za kishirikina.

Vile vile Mchezaji Clement Mzize wa klabu ya Yanga ametozwa faini ya Tsh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kuonekana akiondoa taulo la mlinda mlango wa klabu ya Dodoma Jiji lililokuwa limewekwa kwenye lango la klabu hiyo wakati mchezo ukiendelea, jambo lililoashiria imani za kishirikina.