TATIZO NI UZALISHAJI WA PAMBA SIYO BEI -NYONGO

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Haroon Nyongo, amesema changamoto kubwa katika sekta ya kilimo siyo bei ya mazao kama pamba, bali ni kiwango kidogo cha uzalishaji ambacho kinawaathiri wakulima wengi nchini.

Akizungumza Wakati wakujibu Hoja za wabunge amesema kuwa tafiti zilizofanyika zimeonesha kuwa kwa wastani, hekta moja inazalisha kilo 150 hadi 300 za pamba, hali ambayo haiwezi kumpatia mkulima kipato kikubwa hata kama bei ya kilo moja ingefikia Shilingi 5,000.

Amesema suluhisho ni kuongeza uzalishaji kufikia angalau kilo 1,000 kwa hekta pamoja na kuwekeza kwenye viwanda vya kuchakata mazao ili kuongeza thamani na tija kwa mkulima huku akionya baadhi ya wanasiasa wanaotumia kilimo cha pamba kama ajenda ya kisiasa kwa kudai serikali iongeze bei, badala ya kutoa elimu ya kuongeza uzalishaji na thamani ya mazao.

Kuhusu hali ya uchumi, Nyongo amesema kuwa Tanzania imeendelea kuimarika kiuchumi, ambapo pato la taifa limekua kwa asilimia 5.1 mwaka 2024, ikiwa ni matokeo ya mipango madhubuti ya maendeleo na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *