Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), umepewa Siku 30 za Uchunguzi ili kubaini zilipo fedha za wanufaika zilizolipwa bila kuwafikia walengwa na kufahamu kiwango halisi cha fedha zilizopotea kwa mtindo huo.

Maagizo yametolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene.
amesema “Serikali ipo, hela inapoteaje? Fedha zifuatiliwe hadi katika Kampuni za Simu ambapo kuna namba zinazodaiwa zilikosewa wakati wa kutuma fedha.” Hivi Karibuni, Wadau Walilalamika Uwepo Wa Mazingira ‘Tata’ Ya Ulipaji Kwa Wanufaika Wa Mfuko Huo, Pamoja Na Kudai Malipo Yanafanyika Kwa Watu Ambao Sio Wanufaika Halisi Katika Baadhi Ya Maeneo Nchini Ikiwemo Arusha Na Tanga.