Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Tarura waanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Daraja la mawe lenye urefu wa mita 45 Mkoani Shinyanga

Katika kuhakikisha ufumbuzi unapatikana katika maeneo korofi yaliyokuwa hayapitiki katika Mkoa wa Shinyanga, wakala wa barabara za vijijni na mijini (TARURA) katika mkoa huo tayari wameanza maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa daraja la mawe lenye urefu wa mita 45 litakalounganisha wakazi wa kata ya old Shinyanga na Chibe katika halimashuri ya manispaa ya Shinyanga.

Akizungumzia ujenzi huo Meneja wa TARURA Mkoa wa Shinyanga Avith Theodory amesema, daraja hilo litagharimu Zaidi ya shilingi milioni 120 lengo ikiwa ni kuimarisha mawasiliano kati ya kata hizo mbili na kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kurahisisha muingiliano wa ufanyaji biashara na ,mahusiano ya jamii kwa ujumla

Aidha katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita TARURA wamefanikiwa kujenga daraja la uzogore-Bugwandege katika kata ya Ibadakuli lililogharimu Zaidi ya shilingi milioni 426, na madaraja mawili ya Ibinzamata – kitangiri yenye thamani ya shilingi milioni 2 pamoja na kivuko cha shilingi milioni 100 katika daraja Upongoji_Ndala ndani ya Halmashauri ya Shinyanga.

Tarura wamefanikiwa pia kutengeneza madaraja mawili katika eneo la ndembezo (machinjioni)_seseko,pamoja daraja lingine lililoko katika mtaa wa dome_mwanoni katika kata ya ndembezi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambalo yamegharimu shilingimilioni 50 na daraja lingine katika kanisa la machimu kwa Roja maeneo ya tambukareli kwa gharama ya shilingi milioni 50.

Uimarishaji wa miundombinu ya barabara na madaraja ni mojawapo ya utekelezaji ya ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020/2025 hali inayopelekea kuchochea ongezeko la uchumi kwa mtu mmoja mmoja na ustawi wa jamii kwa ujumla

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *