Tasnia ya Filamu Nchini (Bongo Movie), imepata pigo baada ya kuondokewa na Muigizaji nguli Hashim Kambi, ambaye amefariki ghafla hii leo, baada ya kuanguka akiwa katika majukumu yake ya kikazi.
Hashim Kambi anakumbukwa mchango wake katika soko la filamu nchini, ambapo aliweza kugusa maisha ya wengi kupitia sanaa ya maigizo.

Itakumbukwa kuwa Hashim Kambi aliwahi kuwa mwanasoka nguli, akiichezea Klabu ya Soka ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam na MUNGU ampumzishe kwa amani.


