TANZIA: JOB NDUGAI AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa Spika na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia, leo Agosti 6, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson imeeleza kuwa, msiba umetokea Dodoma

Dkt. Tulia ameeleza kuwa Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *