Tanzania yasitisha Matumizi ya Dawa ya Watoto yenye Utata

Mamlaka za kudhibiti dawa za Tanzania, Rwanda na Zimbabwe zimesitisha toleo la dawa za kikohozi za watoto za kampuni ya Johnson & Johnson, kama hatua ya tahadhari baada ya mamlaka za Nigeria kusema vipimo vilionesha kuwepo na kiwango kikubwa cha sumu.

Nchi hizo zinaungana na Nigeria, Kenya na Afrika Kusini kuondoa dawa hizo madukani, ambazo hutumika kutibu kikohozi kwa watoto. Afrika Kusini imesitisha matokeo zaidi limesema shirika la habari la Reuters.

Vipimo vya maabara kwenye dawa hizo vilivyofanywa na mamalaka ya udhibiti wa dawa ya Nigeria ilionesha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kemikali ya diethylene glycol, ambayo imehusishwa na vifo vya watoto kadhaa nchini Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu mwaka 2022.

Toleo hilo la Benylin lililoondolewa madukani lilitengenezwa na kampuni ya J&J ya Afrika Kusini Mei 2021, ingawa kampuni ya Kenya ya Kenvue sasa inamiliki aina yake.

Mamlaka ya udhibiti wa dawa ya Tanzania -TMDA- ilisema ilianza kusitisha matumizi ya dawa hizo Aprili 12 baada ya kusikia kuhusu matokeo ya vipimo vya Nigeria.

“Zoezi hili halihusishi uchunguzi bali kufuatilia mwenendo na kuhakikisha dawa zenye hitilafu zinaondolewa madukani,” msemaji wa TMDA Gaudensia Simwanza aliiambia Reuters siku ya Jumatatu.

Msemaji wa mamlaka ya Kenya alisema matokeo ya vipimo kwenye dawa hiyo huenda yakatolewa siku ya Jumatano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *