
Klabu ya Tanzania Prison imesitisha mkataba wa kocha Freddy Felix Minziro kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa klabu hiyo uongozi unamshukuru kocha Minziro kwa mchango wake toka ajiunge na kikosi hicho toka 17.7.2023 jijini Mbeya hadi siku ya leo 21.11.2023.
Tanzania Prison ipo nafasi ya 14 kati ya timu 16 katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara wakiwa na alama 7 katika michezo 9 waliyocheza na kushinda mechi moja (1), sare mechi nne (4) na kupoteza mechi nne (4) wamefunga magoli tisa (9) na kufungwa magoli 15.
Kupitia taarifa hiyo kocha Shabani Mtupa amekabidhiwa timu Hadi maamuzi mengine yatakapitangazwa.