Tanzania ni sehemu salama ya uwekezaji 

Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko amesema Serikali itaendelea kuleta mitambo kwa ajili ya uchorongaji ili kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini.

Amesema Serikali itaendelea kufanya hivyo huku ikiboresha mazingira ya uwekezaji kwa wachimbaji wakubwa.

Dkt. Biteko ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Jukwaa la Uwekezaji Sekta ya Madini Tanzania.

Amesema Serikali itafanya hivyo ili taarifa za kijiolojia walizonazo wachimbaji wadogo zitokane na sayansi iliyopatikana kwenye uchorongaji.

Aidha, Dkt. Biteko amewatoa hofu Wawekezaji waliopo nchini na nje ya nchi kwa kusisitiza kuwa Tanzania ni sehemu salama ya uwekezaji na hapatakuwa na urasimu wala ucheleweshaji linapotokea suala la uwekezaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *