Kwa mujibu wa Global Mind Project, nchi ya Tanzania imetajwa kuwa nchi yenye furaha zaidi barani Afrika,

Tanzania ambayo inapatikana Ukanda wa Afrika Mashariki imekuwa na kiwango cha Afya ya Akili (MHQ) kinatumika katika ripoti hii kupima ustawi wa akili, huku Tanzania ikipata alama za juu zaidi za 88.
Nchi zingine 10 za Kiafrika zimepata alama za MHQ na kuzidi 60, zikionyesha ustawi mzuri wa kiakili kwa ujumla katika bara zima. Nigeria na Zimbabwe zinaifuata Tanzania kwa karibu kwa alama 83 na 74 kwenye MHQ.