Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Tanzania kuimarisha  biashara ya mawasiliano kwa kuwekeza katika mkonge wa taifa

Imeelezwa kuwa Tanzania ina mpango wa kuimarisha biashara ya mawasiliano kwa kuendelea  kuwekeza katika mkongo wa taifa ili kusambaza huduma za mawasiliano nchini na hatimaye kuuza huduma hiyo kwa nchi jirani zisizokuwa na milango ya bahari ili kuongeza mapato ya nchi kupitia sekta ya mawasiliano.

Hayo yameelezwa na waziri wa habari na tekinolojia ya mawasiliano Nape Nauye wakati akitoa taarifa kwa kamati ya kudumu ya bunge ya miundo mbinu iliyofika mkoani Shinyanga ili kukagua utekeleaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kwa fedha zilizoidhinishwa na bunge, ambapo mojawapo ya miradi hiyo ni mkongo wa taifa kituo cha shinyanga.

Aidha kamati hiyo pia imekagua ujenzi wa kiwanja cha ndege kilichopo katika kata ya Ibadakuli halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ili kuona utekelezaji wake ambapo waziri wa ujenzi Inocenti Bashungwa ameimbia kamati hiyo kuwa mradi huo unaendelea vizuri huku suala la unufaishaji wananchi kupitia mradi huo (CSR) likiendelea kuzingatiwa kwa mujibu wa maelekezo ya serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *