Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia 2024 Tanzania ndilo Nchi yenye deni dogo la Taifa dogo ikilinganishwa na wastani wa deni hilo kwa nchi zote za Afrika Mashariki na kwamba deni zima la mataifa yote duniani limefika asilimia 93.
Dkt. Samia ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameyasema hayo hii leo Agosti 28, 2025 katika ufunguzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) kitaifa, zilizozinduliwa katika viwanja vya Tanganyika Pakers, Jijini Dar es Salaam.

Amesema, “deni la taifa hadi kufikia mwaka 2024, Deni la serikali zote duniani lilikuwa asilimia 93 ya pato lote la dunia ukichukua serikali zote za dunia, wakati pato la serikali zote za Afrika lilikuwa silimia 67 ya pato lote ndani ya bara la Afrika, kwa ukanda wa Afrika Mashariki deni hili lilifika asilimia 67 kwa wastani wa pato la taifa kwa nchi zote za Afrika Mashariki.”
Ameongeza kuwa, kwa nchi mojamoja Tanzania ilisalia kuwa asilimia 46 ya pato la Taifa ambalo ni ndilo deni dogo kuliko yote kwa nchi za Afrika Mashariki kwa asilimia 46, ukilinganisha na washtani wa asilimia 67.


