Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) imewazuia wananchi kutumia madaraja ya juu maarufu kama ‘flyover’ isivyotakiwa kama kupita kwa miguu juu ya madaraja hayo au kupiga picha mnato( selfie), kupiga picha za harusi na kufanya mazoezi katika madaraja hayo .
Hayo yamesemwa na Meneja wa kitengo cha usalama barabarani kutoka TANROADS makao makuu Mhandisi George Daffa akitoa elimu sahihi ya kutumia madaraja hayo kwa watembea kwa miguu na wanamichezo.
“Kuna wengine wanafanya mazoezi kule kwenye madaraja ya juu ni kujihatarisha usalama wako,vilevile kuna watu wengine wanafanya mazoezi na kutembea katika daraja la Tanzanite sehemu ya magari yanapopita ile hairuhusiwi sababu unaweza pata shida ya kugongwa na gari”
“Kutokana na sheria hawaruhusiwi kufanya mazoezi mule utakapo kamatwa unatembea katika barabara za magari, au kupaki gari lako na kupiga selfii unachukuliwa sheria kwa mujibu wa sheria za barabara zinavyosema” – Mhandisi Daffa.