TANESCO YATOA MAELEKEZO YA KUNUNUA LUKU..

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kuna changamoto katika manunuzi ya meme na inasababisha wateja kushindwa kununua umeme kupitia mitandao ya simu na njia za kibenki kuanzia leo majira ya saa tatu asubuhi.

Hivyo, Shirika linawashauri wateja kufanya manunuzi ya umeme kupitia kwa Mawakala wetu walioko nchi nzima wakati wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kurekebisha changamoto iliyojitokeza ili kuwezesha manunuzi ya umeme kwa mitandao ya simu na njia za kibenki kurejea kwenye hali yake ya kawaida.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *