NA EUNICE KANUMBA –UKENYENGE KISHAPU
TAMASHA la jadi ambalo hufanyika kila mwaka kwa kuwakutanisha wanajamii katika himaya ya utawala wa Busiha linalojulikana kama sanjo ya Busia limezinduliwa rasimi kwa mwaka huu 2025 na kiongozi wa himaya hiyo chifu Makwaia wa tatu katika makazi yake yaliyopo kata ya Ukenyenge halimashuri ya wilaya ya Kishapu,mkoani Shinyanga.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Tamasha hilo chifu Makwaia wa tatu ambaye ni kiongozi wa 24 wa himaya hiyo ameitaka jamii ya wasukuma kujivunia mila, desturi na tamaduni zao ambazo zmerithiwa kutoka kwa mababu kama sehemu ya kuzienzi na kuacha alama kwa vizazi vijavyo, na kwamba mila hizo hazipaswi kupuuzwa kwani hazajachakachuliwa kwa kuchanganywa na tamaduni za kigeni.

Kwa upande wao Washiriki wa tamasha hilo kutoka vikundi mbalimbali vya ngoma za asili ya Kisukuma wameeleza tija ya uwepo wa matamasha hayo hususani kutunza mila la tamaduni zilizoachwa na mababu na kujikwamua kiuchumia kupitia michezo wanayoshiriki.

Waratibu wa tamasha hilo na shuguli za utemi wa Busiya wamesema matamasha hayo yamekuwa yakisaidia kuwaunganisha jamii ya wasukuma kupitia michezo mbalimbali ambayo imekuwa ikijumuishwa katika tamasha hilo linalofanyika kwa mwaka wa 16 mfululizo
Tamasha hilo la kitamaduni limekuwa likitumika kama jukwaa la kuonyesha utamaduni wa msukuma kwa shuguli zinazofanywa ikiwemo Ngoma, mavazi ya asili ,michezo ya asili vyakula vya asili huku shughuli hizo zikitarajiwa kuhitimishwa kesho July 7 2025 katika viwanja vya makazi ya chifu wa busiya.