Takukuru Yawataka Viongozi wa Dini Kukemea Rushwa

Na Melkizedeck Anthony,Mwanza

Viongozi wa dini mkoani Mwanza wametakiwa kukemea vitendo vya rushwa hususani katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea katika uchaguzi wa serikiali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani.

Rai hiyo imetolewa Agosti 29,2024 na mkuu wa dawati la kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Bi. Stela Bukuru wakati akiwasilisha masa katika mafunzo kwa viongozi wa dini pamoja wazee wa mkoa wa Mwanza ambapo amesema katika nyakati za uchaguzi kumekua na vitendo vya rushwa ambapo kwa mujibu wa uchambuzi uliofanyanywa na taasisi hiyo ulibaini kuwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014 na 2019 kulikua na ugawaji wa fedha taslimu, doti za kanga, tisheti pamoja na vyakula huku pia kukiwa na ahadi za mikopo na upendeleo maalumu kwa wapiga kura endapo wagombea waliofanya hivyo watachaguliwa.

Bi.Stela pia amesema katika uchaguzi huo pia kulikua na matumizi ya lugha za vitisho ambapo moja ya sehemu ambayo kulionekana kuwa na viatarishi vya rushwa ni wakati wa kujiandikisha na maandalizi ya orodha ya wapiga, wakati wa uteuzi wa wagombea pia wakati wakati wa kampeni za wagombea  na hivyo ili kuepuka yote viashiria vyote hivi vya rushwa viogozi wa dini wanapaswa kushiriki katika kukemea vitendo vya rushwa pale wanapokua katika maeneo yao ya ibada.

Kwa upande wake Afisa uchaguzi wa halmashauri ya jiji la Mwanza Francisca Mshashi amesema katika kipindi hiki ambacho taifa linakwenda katika uchaguzi viongozi wa dini wananapaswa kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuwachagua viongozi wanaowataka huku pia wakizingatia suala la amani na utulivu pale wanapokua katika uchaguzi huo ili uweze kumalizika salama.

Awali akifungua mafunzo hayo mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mwanza James Ruge amesema rushwa ni kosa la kimaadili, kiimani na kijinai na hii ni kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura namba 329 na marejeo yake ya mwaka 2022 na ndio maana serikali imeona upo umuhimu wa kuzungumza na viongozi wa dini kwani wanayo nafasi ya kukutana na waumini wao na kuwahimiza juu ya umuhimu wa kufanya uchaguzi huku wakijiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaweza kujitokeza katika kipindi cha uchaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *