TAKUKURU YATOA ELIMU YA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA, DAWA ZA KULEVYA KWA WALIMU SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI


Na Daniel Gahu – Katavi.

Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi, imeendesha mafunzo Kwa Walimu walezi wa vyama vya kupinga rushwa na Vitendo viovu mashuleni (PCCB) Kwa shule za msingi na secondary zinazopatikana ndani ya Manispaa ya wilaya ya Mpanda.

Mafunzo hayo yamefanyika leo tarehe 20 June, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya wilaya ya Mpanda na Kuongozwa na mgeni rasmi, Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda bi Sophia Kumbuli amesema, dhumuni kubwa la mafunzo hayo ni kutoa elimu Kwa Walimu walezi wa shule zote ndani ya Manispaa ya Mpanda, kwani Walimu ndio walezi wa watoto mashuleni na hutumia muda mwingi kuwa na watoto kuliko hata wazazi wao.

Akiendelea kuzungumza mbele ya kamanda wa TAKUKURU mkoa amesema mafunzo hayo yatajikita zaidi juu ya uepukaji wa matumizi ya madawa ya kulevya, Vitendo vya rushwa, ubakaji na ulawiti. Sambamba na hayo zaidi amehimiza uzalendo na uadilifu Kwa nchi ya Tanzania hasa kuelekea katika kipindi Cha uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais.

Aidha, Kamanda wa Mkoa wa Katavi kutoka Taasisi ya kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU), Sipha Nkusi Mwanjala nae amebainisha kuwa Kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya tisa(H) inaelekeza, taasisi za nchi,mamlaka za usimamizi na nchi kwa ujumla zinapaswa kuelekeza juhudi zake zote katika kutokomeza Rushwa nchini.

Pia amesema, “mapambano dhidi ya rushwa na Vitendo vyote viovu sio vya nchi tu bali niyakila mmoja wetu. Hata hivyo Sheria ya kupambana na Rushwa sura ya 329, marejeo ya mwaka 2022 inaipaTakukuru majukumu yakuongoza na kupambana na Rushwa nchini pamoja nakushirikisha wadau mbalimbali mkiwemo nyie Walimu walezi mlioko hapa”.

Mnamo mwaka 2007, Takukuru ilifungua kampeni za kuanzisha club za kupinga rushwa mashuleni katika shule za secondary na msingi, na mnamo mwaka 2013 club hiyo ilianzishwa katika shule za misingi zote nchini na kwasasa club hizo zipo katika vyuo vya kati na vikuu.

Akihitimisha kamanda wa Takukuru, amewataka Walimu walezi kutumika kama daraja la kufikisha elimu hii adhimu ya mapambano dhidi ya rushwa Kwa wanafunzi wote walioko mashuleni ili kutengeneza vizazi vyenye uadilifu na matendo mema kwani kupitia watoto waliopo mashuleni ndio hutoka viongozi wa badae na kwakufanya hivyo tutatengeneza Taifa lenye manufaa na maendeleo katika vizazi vyote.

Kwa upande wao walimu, wakiongozwa na Mwalimu Haruna Yusuf kutoka shule ya msingi Kashato amesema, wao kama Walimu watahakikisha elimu hiyo inawafikia wanafunzi wote juu ya kupambana na maswala ya Rushwa na madawa ya kulevya na kutengeneza kuzazi chenye manufaa kwa Taifa letu teule la Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *