Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga,imembana Mkandarasi kutoka Kampuni ya Brampem Global Investment LTD, kurudia matengenezo ya barabara aliyojenga chini ya kiwango, pamoja na kukatwa fedha kutokana na kuchelewesha matengenezo hayo kinyume cha mkataba.
Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja, amebainisha hayo leo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa kipindi cha robo ya Nne ya mwaka wa fedha 2022/2023.
Amesema kwa kipindi hicho walifanya ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ikiwamo ya matengenezo ya barabara, zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga chini ya usimamizi wa TARURA ili kuona utekelezwaji wa miradi hiyo kama imezingatia ubora na viwango vinavyotakiwa.
Amesema katika ufuatiliaji wa matengenezo ya barabara hizo kwa uboreshaji wa vipande vya barabara katika Kata ya Chamaguha, Ngokolo, Ndembezi, Kambarage na Mwasele, walibaini Mkandarasi kutekeleza ujenzi wa barabara hizo chini ya kiwango. Endelea kutufuatilia zaidi kupitia (TAKUKURU) mkoani Shinyanga,imembana Mkandarasi kutoka Kampuni ya Brampem Global Investment LTD, kurudia matengenezo ya barabara aliyojenga chini ya kiwango, pamoja na kukatwa fedha kutokana na kuchelewesha matengenezo hayo kinyume cha mkataba. Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja, amebainisha hayo leo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa kipindi cha robo ya Nne ya mwaka wa fedha 2022/2023.
Amesema kwa kipindi hicho walifanya ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ikiwamo ya matengenezo ya barabara, zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga chini ya usimamizi wa TARURA ili kuona utekelezwaji wa miradi hiyo kama imezingatia ubora na viwango vinavyotakiwa. Amesema katika ufuatiliaji wa matengenezo ya barabara hizo kwa uboreshaji wa vipande vya barabara katika Kata ya Chamaguha, Ngokolo, Ndembezi, Kambarage na Mwasele, walibaini Mkandarasi kutekeleza ujenzi wa barabara hizo chini ya kiwango.