Na Saada Almasi – Simiyu.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Simiyu imenusuru zaidi ya Bilioni sita za miradi ya sekta ya elimu iliyojengwa chini ya kiwango.
Akiongea katika uwasilishwaji wa ripoti ya robo ya tatu ya fedha ya mwaka 2025/2026 mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo, Manyama Tungaraza amesema kuwa kati ya miradi iliyokuwa imefanyiwa ubadhirifu ni pamoja na ule wa shule ya sekondari ya wavulana Simiyu ambapo baadhi ya miundombinu ya mradi huo ilijengwa juu ya bomba la maji safi hatua iliyopelekea mradi huo kuchelewa kwa takribani siku 119.

“Mradi wa shule hii unathamani ya shilingi bilioni 4.1 na ulianza kujengwa mwezi Oktoba 2024 kwa matarajio ya kukamilika mwezi Aprili 2026 baada ya kukagua na kubaini hivyo tulikaa kikao na wadau wakasitisha ujenzi ili kulihamisha bomba hilo ambalo lingeweza kuleta madhara na gharama baadae na tulifanikiwa kulihamisha kwa mantiki hiyo kukamilika kwa mradi huo wa shule unatarajiwa mwezi Julai 2025,” amesema Manyama
Mradi mwingine ni ule wa shule ya sekondari Kabondo kata ya Kabondo wilayani Meatu wenye thamani ya shilingi milioni 584 baada ya fundi ujenzi wa shule hiyo aliyepewa mkataba wa siku 90 kushimdwa kutimiza kusudio kwa wakati.

“Timu ya ufuatiliaji wa mradi huu ilibaini utekelezwaji wa mradi kwa asilimia kumi tu licha ya kipindi cha siku 90 yaani tangu Oktoba 24 2024 na kupaswa kukamilika Januari 24 2025 kuisha kutokana na fundi aliyeshinda zabuni hiyo kutokuwa na fedha za kumaliza kwa hivyo fundi mwingine ametafutwa na tayari kamaliza mradi”
Sambamba na hilo Tungaraza amesema kuwa TAKUKURU mkoani humo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi wa mkoa huo kupitia TAKUKURU Rafiki juu ya namna ya kujiepusha na vitendo vya rushwa na kuendelea kutoa ushirikian na taasisi hiyo ili kuiweka jamii salama