Mkuu wa Wilaya ya Geita Cornel Magembe ameiagiza TAKUKURU Wilaya ya Geita kufanya uchunguzi wa kina juu ya fedha zilizotumika katika safari ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Zahara Michuzi kama amekwenda kwa maslahi ya Halmshauri na ikibainika ameenda kwa maslahi binafsi basi fedha zilizotumika zirudishwe kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo.
Amezungumza hayo katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji wa Geita ambapo amesema Halmashauri hiyo imekuwa ina changamoto ambayo lazima Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita asimame kwa umakini hayupo tayari kuonekana hawajibiki.
Madiwani wametakiwa pia kukubaliana ikiwa kuna Baraza Mkurugenzi awepo na kama hayupo liahirishwe.