Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Takriban Watu 100 Nchini Nigeria Wapoteza Maisha Kwa Mripuko Wa Lori La Mafuta

Chanzo: DW

Takriban watu 94 wameteketea hadi kupoteza maisha na wengine 50 wakiwa katika hali mbaya kufuatia moto mkubwa uliosababishwa na mlipuko wa lori la mafuta usiku wa kuamkia octoba 15 katika Jimbo la Jigawa Kaskazini Magharibi mwa Nigeria.


Polisi wameeleza kuwa wengi wa walioathiriwa walikuwa wakijaribu kuchota mafuta yaliyomwagika baada ya lori kuanguka katika mji wa majia jimbo la jigawa.


Chama cha madaktari nchini Nigeria kimewataka wahudumu wa afya kuwasili haraka kwenye vituo vya dharura vilivyo karibu na eneo hilo ili kusaidia kutoa huduma kwa idadi kubwa ya majeruhi.


Ajali kama hizi zimekuwa zikitokea mara kwa mara nchini nigeria na kusababisha vifo vya mamia ya watu.


Mwezi uliopita, takriban watu 48 walipoteza maisha wakati lori la mafuta lilipogongana na gari lingine katika jimbo la kati la niger.

Vilevile mwezi julai 2023, lori la mafuta liliripuka katika jimbo la Ondo Kusini Magharibi mwa Nigeria na kuua watu wasiopungua nane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *