Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Taka tishio la afya wakazi wa Luchelele

Baadhi ya Wananchi wa kata ya Luchelele wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya usafi wa mazingira katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa uzoaji wa taka ili kuwanusuru na magonjwa ya milipuko.

Wakizungumza na Jambo FM baadhi ya wananchi hao wao wamesema katika kata hiyo bado utaratibu wa uzoaji wa taka sio mzuri kwani taka hizo zimekua zikichelewa kuzolewa jambo linalowasukuma kuiomba serikali kupitia mamlaka husika kuweka utaratibu mzuri wa uzoaji wa taka hizo ili kuwanusuru wananchi na madhra ya taka hizo.

Akitolea ufafanuzi kwa njia ya simu, Afisa Mazingira wa halmashauri ya jiji la Mwanza Fanuel Kasenene amewataka wananchi wa kata hiyo kutoa ushirikiano kwa mawakala wanaohusika na uzoaji wa taka hizo kwa kuwa utaratibu wa kutupa taka katika maeneo yalioainishwa na mawakala hao ili mazingira yawe safi wakati wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *