Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amesema kuwa mchezo wao kesho dhidi ya DR Congo, Tanzania inaenda kushinda na kuondoka na alama tatu muhimu.

Samatta amesema hayo katika mkutano na wanahabari leo, ambapo amebainisha kuwa baada ya mchezo ule, tayari wao kama wachezaji wamezungumza na kurejeshana mchezoni, ili kuingia na kiwango bora zaidi katika mchezo wa kesho.
“Kama tuliamini tungeweza kupata ushindi dhidi ya Zambia, basi inawezekana hivyohivyo katika mechi na Congo……wachezaji wote wanaelewa umuhimu wa mchezo wa kesho na nini tunachotakiwa kukifanya, kwahiyo tunakwenda kupambana kuhakikisha tunapata ushindi”


