Timu za Manispaa ya Tabora zimeendelea kujiweka pazuri kwenye msimamo wa Makundi Katika michezo ya Watumishi wa Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA) inayoendelea jijini Mbeya.
Katika michezo minne ambayo timu za Manispaa ya Tabora zimecheza, zimeshinda michezo mitatu na kupoteza mchezo mmoja.

Matokeo ya michezo hiyo yako kama ifuatavyo;
TABORA MC 26 Vs 22 ARUSHA CC ( Basketball Wanaume),
TABORA MC 4 Vs 3 KAHAMA MC (Handball Wanaume),
TABORA MC 7 Vs 2 TUNDURU DC (Handball Wanaume),
TABORA MC 0 Vs 1 KAHAMA MC (Football Wanaume).




