TABOA “nauli za mabasi zipande”

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imewaonya watoa huduma ya usafirishaji wa abiria mijini (daladala) kupandisha nauli kinyemela na kuwataka kufuata utaratibu uliowekwa.

LATRA imeitisha mkutano wa wadau kwa ajili ya kupokea maoni kuhusu marejeo ya nauli za mabasi ya masafa marefu na daladala mkoani Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa TABOA, hoja kubwa watakayowasilisha kwenye kikao hicho ni kuomba nauli zipandishwe ili kuwasaidia kumudu gharama ambazo zimepanda ili kuendelea kutoa huduma bila matatizo.

Katibu Mkuu wa TABOA, Priscus Joseph, alisema sababu kubwa ya kuomba kupandishwa kwa nauli ni kupanda kwa mafuta, kuadimika na kupanda kwa dola na kupanda kwa gharama za vipuri vya magari ambavyo asilimia kubwa huagizwa nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *