Na Saulo Stephen – Singida.
Taasisi za Serikali na Taasisi binafsi Nchini, zimetakiwa kujitokeza katika kusaidia makundi yenye mahitaji malaamu ikiwemo watu wenye ulemavu ili kuwa sehemu ya faraja kwa Makundi hayo.
Wito huo, umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete wakati wa zoezi la kukabidhi Viti Mwendo vilivyotolewa na WCF kwa wanafunzi wenye Ulemavu wanaosoma katika Chuo cha watu wenye mahitaji maalumu kilichopo mkoani Singida.

Amesema Viti mwendo hivyo vitawasaidia wanafunzi hao kuweza kujonge sio tu kipindi watakapo kuwa chuoni lakini pia vitawasaidia hata watakapomaliza masomo yao nakwenda kufanya shughuli mbalimbali katika Jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Omari Dendego ameushukuru uongozi wa WCF kwa kuamua kuchagua mkoa wa Singida na chuo cha Sabasaba kwa ajili ya msaada huo wa viti mwendo kwa wanafunzi hao,kwani wangeweza kwenda mkoa wowote kati ya mikoa 26 Nchini lakini wameamua kuuchagua Mkoa wa Singida.

Nae Mkurugenzi wa mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi Nchini WCF, Dkt. John Mduma amesema lengo la kutoa viti hivyo ni kuhakikisha wanafanya wanafunzi hao waweze kusoma masomo yao vizuri kwa kuwarahisishia huduma ya kujongea kupitia viti mwendo hivyo.