Ofisi ya Rais TAMISEMI imekanusha taarifa zilizotolewa na Sifaeli Tawel Elirehema za kwamba alinyang’anywa haki yake ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano katika shule ya sekondari Namwai. Kwani matokeo yake alipata div IV :34 (Zero) na alikuwa mchepuo wa masomo ya sanaa na si sayansi kama taarifa zilivyosambaa.
Hayo yamebainishwa baada ya taarifa kusambaa mitandaoni zikionesha binti huyo kusema yeye alipata division 1:10 na nafasi yake alipewa mtu mwingine jambo ambalo si la kweli.
