T.I na mkewe washtakiwa kwa kufanya unyanyasaji

Rapa T.I. na mkewe Tiny Harris wanashtakiwa na mwanamke aliyetambulikwa kwa jina la Jane Doe kwa kosa la kumnywesha dawa za Kulevya na kumfanyia unyanyasaji wa kingono mnamo mwaka 2005 .

Mwanamke huyo anasema kuwa alikuwa kwenye sherehe nyumbani kwa Coolio na kukutana na mwamaume aitwaye  “Caviar”, ambaye, alidai kuwa anafanya kazi kwa T.I.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ  mlalamikaji anasema kuwa kwenye sherehe hiyo akumuona T.I wala mkewe ila  “Caviar” alimwambia wangekuwa wote kwenye klabu ya usiku ya L.A. usiku uliofuata, na ndipo walipokutana wote … katika sehemu ya VIP na kupewa kinywaji na Mke wa T.I ambacho alikunywa na kujikuta kwenye chumba cha Hoteli akiwa na rapa huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *