Rapa Kendrick Lamar amegonga headline kufuatia onyesho lake Super Bowl Half Time Show 2025, ambalo ilishuhudiwa na watu kibao huko Jiji la Kansas, huku akiwashangaza raia kwa tumbuiza wimbo wa Diss wa Drake “Not Like Us,” “squabble up,” “HUMBLE.” na “luther.”
Onyesho hilo lilianza kwa utangulizi kutoka kwa mwigizaji Samuel L. Jackson, aliyevalia vazi lililoongozwa na Mjomba Sam, akisema, “Ni Mjomba wako Sam na huu ni mchezo mzuri wa Marekani.”

Nyota huyo wa muziki wa hip-hop mzaliwa wa Compton aliendelea kufanya majabu kwa dakika 13 na baadhi ya vibao vyake vikubwa zaidi, vikiwemo, “squabble up,” “HUMBLE.,” “GNX,” “Tv off.”
Onesho hilo, lilihudhuriwa na ma’ Star kibao akiwemo Serena Williams aliyeonekana jukwaani wakati wa onyesho hilo la Super Bowl Half Time Show, akiwa na SZA, Mustard na Samuel L. Jackson.