Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Sungusungu sita wahukumiwa kunyongwa baada ya kuhusika na mauaji

Mahakama Kuu masjala ndogo ya Manyara, imewahukumu adhabu ya kifo walinzi sita wa jadi ‘Sunsusungu’ bada ya kupatikana na hatia ya  kumuua  kikatili mtu waliyemtuhumu kuwa mwizi wa mifugo.

Maelezo ya onyo ya kukiri kosa la  washtakiwa wote sita waliyoyaandika polisi kwa hiyari yao, ndiyo ushahidi mzito uliowatia hatiani kutokana na maelezo hayo kueleza hatua kwa hatua tangu walipomkamata marehemu na kisha kumuua.


Katika hukumu hiyo iliyotolewa  na Jaji Gladys Barthy na nakala yake kupatikana katika mtandao wa Mahakama leo Alhamisi, Machi 7, 2024, imesema kuwa Mahakama iliwaachia huru sungusungu watatu kwa kukosekana ushahidi dhidi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *