STEPHANE AZIZ KI APEWA ‘THANK YOU’ YANGA SC

Klabu ya Yanga imetangaza kuachana rasmi na mchezaji wake, Stephane Aziz Ki baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu akitokea Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Hatuq hiyo inakuja kufuatia Klabu ya Wydad Casablanca kukamilisha uhamisho wa kiungo huyo shambuliaji kwa Mkataba wa miaka miwili.

Wydad inajiandaa na michuano ya Kombe la Dunia la Klabu na imeongeza wachezaji watatu kikosini akiwemo Nordin Amraba na Hamza Hanoun.

Baada ya taarifa ya Yanga, Aziz Ki kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amewaaga wananchi akisema, “Moyo wangu ni mzito kuwapa taarifa ya kuhusu kuondoka kwangu kwenye klabu ya moyo wangu, Yanga ni zaidi ya klabu.”

“Yanga imenitengeneza na kunijenga, Yanga imenipa sehemu yangu ya pili ya nyumbani na imenipa mke mzuri,” alimaliza Aziz Ki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *