Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Hemed Suleiman amekitaja Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, kitakachoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Tanzania itacheza mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Morocco Machi 26, 2025 ugenini, ambapo Nahodha Mbwana Samatta anayekipiga huko PAOK ya Ugiriki ataukosa mchezo huo kwani ana majeraha.