Serikali imewaahidi wachezaji na benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kiasi cha Tsh Bilioni 1.3 endapo itafuzu hatua ya 16 bora ya fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Taifa Stars leo itapambana na DR Congo katika mchezo wa mwisho wa kundi F, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro amesema ahadi hiyo ya fedha imetolewa ili kuongeza hamasa kwa wachezaji.