NA EUNICE KANUMBA – SHINYANGA
Mechi ya Stand United na Fountain Gate imemalizika katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.
Mchezo huo ni wa Kwanza wa Playoff ambapo mchezo wa marudiano utachezwa huko Manyara tarehe Julai 8, katika uwanja wa kwaraa uliopo mjini humo, ambapo mshindi atashiriki kucheza msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Goli la kwanza la Fountain Gate limefungwa kipindi cha kwanza na mchezaji Kasim Haroon katika dakika ya 28 ,huku Stand United wakisawazisha dk ya 44 goli liliofungwa na Joram Mgeveke.

Kipindi cha pili Fountain Gate waliongeza Goli,lililofungwa na Said Sadiki dk 65. ambapo Goli la tatu lilifungwa na Mudrick Gonda dk 82. Baada Goli hilo kufungwa, iliibuka vurugu na kusababisha mpira kusimama kwa muda.
Hadi dakika 90 zinamalizika Fountain Gate walibakia na Goli zao 3 dhidi ya moja 1 ambalo walipata stand united katika kipindi cha kwanza.