TIMU ya Stand United ya mjini Shinyanga wameibuka na ushindi wa goli 2-0, dhidi ya Geita Gold katika ligi ya Championship.
Mechi hiyo imechezwa leo Mei 29,2025 katika uwanja wa CCM Kambarage uliopo katika halimashauri ya manispaa ya Shinyanga.

Goli la kwanza la Stand United limefungwa na Yusuph Adam dk ya 14 kipindi cha kwanza, ambapo kipindi cha pili Stand United waliongeza Goli la pili kwa mkwaju wa Penati, Goli liliofungwa na Omary Rajabu katika dakika ya 85 baada ya mchezaji Seleman Hassan wa Stand United kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari .

Baada ya ushindi huo ambapo Mechi ilikuwa ya Playoff, Stand United inasubili timu zilizoshika nafasi ya nafasi ya 13 na 14 ambazo ni Fountain Gate na Prison ambapo zitacheza play off na mshindi kusalia ligi kuu na atakayeshindwa atacheza na Stand United ili kupata atakayefuzu rasmi kucheza Ligi kuu kwa msimu ujao.