STAMICO YAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WACHIMBAJI WADOGO

Na Ibrahim Rojala – Geita.

Uchimbaji holela, usawa wa kijinsia na ujumuishwaji wa vijana katika shughuli za uchimbaji wa madini nchini ni miongoni mwa changamoto ambazo serikali kupitia SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO), imeendelea kuzitatua ili kuongeza tija kwa wachimbaji wadogo.

Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO, Deusdedith Magala amebainisha hayo wakati akizungumza na Wachimbaji wadogo wa madini wanaoendesha shughuli zao katika eneo la Ushirombo amkoani Geita, waliokutanishwa na wadau mbalimbali wa sekta ya madini kwenye mkutano maalum ulioandaliwa na Mtandao wa AFINet kwa kushirikiana na Mtajirishaji Media lengo kutoa mbinu za uwekezaji katika uchimbaji madini ambapo pia ameeleza namna shirika hilo linavyotambua mchango wa wachimbaji wadogo.

Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO, Deusdedith Magala.

Mwenyekiti wa AFINet, Aloyce Midelo amesema mkutano huo ulilenga kujenga mahusiano kati yao na wachimbaji wadogo na kampuni yao, taaisisi muhimu zinazotoa huduma muhimu za kuwaendeleza wachimbaji wadogo katika eneo la utafiti na ufundi ili leseni walizonazo ziwezeshe malengo mahususi kufikwa nae Mkuu wa hifadhi ya Kigosi, Yohane Mwampashi ametumai mkutano huo kuelezea mazingira rafiki yaliyowekwa na serikali kwa wachimbaji wanaofanya utafiti wa madini katika pori hilo.

Mkutano huo umehusisha taasisi za kifedha pamoja na mashirika ya umma kama STAMICO, TFS, NSSF na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii, kwa  lengo la kuwawezesha wachimbaji kupitia mafunzo, ushauri na fursa za kifedha, ukiangazia masuala muhimu kama urasimishaji wa shughuli za uchimbaji, upatikanaji wa msaada wa kiufundi na mikakati ya kuendeleza biashara zao kwa tija na uendelevu.

Aidha umefanyika ikiwa ni sehemu ya jitihada zinazoendelea za mradi wa urasimishaji wa biashara za wachimbaji wadogo ulioanzishwa mwaka 2019, ukilenga kuliwezesha kundi hilo(wachimbaji wadogo)kuchangia katika uchumi na mapato yatokanayo na  sekta ya madini  nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *