Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Staa wa Black Panther afariki Dunia

Aliyekuwa muigizaji wa filamu za “Black Panther” na “Avengers”, Taraja Ramsess (41), pamoja na watoto wake watatu wamefariki Dunia kwa ajali ya gari iliyotokea wiki moja iliyopita huko Georgia.

Kituo cha Televisheni cha Atlanta WSB-TV kiliripoti kuwa ajali hiyo ilitokea kabla ya saa sita usiku, siku ya Halloween baada ya gari la Ramsess kugongana na trela ambalo lilikuwa imeharibika barabarani.

Watoto wa msanii huyo waliofariki ni, binti yake wa Sundari(13), kijana wake Kisasi (10) na binti yake mchanga Fujibo mwenye umri wa wiki 8.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *