Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Spika Dkt.Tulia Aagiza Mbunge Mpina Ahojiwe

Na Gideone Gregory,Dodoma

Spika wa Bunge na Rais wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson ameiagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumhoji Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kufuatia kitendo cha Mbunge huyo kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu ushahidi aliouwasilisha kwa Spika juu ya madai aliyoyatoa bungeni kuwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alilidanganya Bunge.

Dkt. Tulia ametoa maelekezo ya leo Juni 18,2024 Bungeni Jijini Dodoma akieleza kuwa kitendo cha Mpina, ambaye ni Mbunge mzoefu anayezifahamu kanuni za Bunge, kuwasilisha ushahidi wake na kisha kwenda  kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu nyaraka za ushahidi huo, ni kitendo cha utovu wa nidhamu kwa Bunge na Spika.

“Pia kitendo hiki ni kudharau mamlaka ya Spika na kuingilia mwenendo wa Bunge na kushusha hadhi na heshima ya Bunge”,amesema.

Itakumbukwa awali Mbunge Mpina alipewa wiki moja kuwasilisha ushahidi wake baada ya kulieleza Bunge kuwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amelidanganya bunge katika sakata la uagizaji wa sukari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *