Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Somalia yajiunga EAC

Somalia imekuwa mwanachama rasmi wa nane wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya mkutano wa wakuu wa nchi za EAC kuidhinisha maombi yake ya muongo mmoja ya kujiunga na jumuiya hiyo ya kikanda.
Jana Ijumaa, viongozi hao wa EAC waliidhinisha uanachama wa Somalia katika umoja huo wakati wa Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Arusha, kaskazini mwa Tanzania.

Somalia inaungana na Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda kuunda jumuiya ya EAC.

Rais Mohamud amewashukuru wakuu wa nchi za EAC kwa imani yao waliyoionesha kwa Somalia na kuidhinisha ombi lake la kujiunga na jumuiya hiyo.

Katika mkutano huo, Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi amekabidhi uenyekiti wa mzunguko wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *