Mtayarishaji wa Muziki toka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Ayo Lizer “lizerclassic” amechapisha andiko kuwa lebo hiyo inatafuta saini za wasanii wapya sita.
Lizer amechapa andiko hilo kunako kurasa yake ya Instagram akisema, “ikiwa wewe ni msanii mwenye kipaji na una sifa zifuatazo, tunakukaribisha kutuma maombi yako.”

‘Prodyuza’ huyo pia ameainisha vigezo vya watumaji wa maombi ikiwemo kujua kuimba vizuri nyimbo za aina tofauti.
Kingine ni uwezo wa kuandika nyimbo kwa ufasaha, kujua kucheza, nyimbo tatu ambazo zilisharekodiwa na maelezo mafupi ya muhusika.
