SITA WAFARIKI KWA AJALI YA BOTI KUZAMA MAJI CANARY

Watu sita wamefariki dunia baada ya boti ya wahamiaji waliyokuwa wakisafiria kuzama karibu visiwa vya Canary, Nchini Uhispania.

Kwa mujibu wa taarifa ya huduma za dharura imeeleza kuwa tukio hilo limetokea hii leo Mei 28, 2025 na kuongeza idadi ya majanga yanayotokea kwenye njia hatarishi za uhamaji.

“Waokoaji wakisaidiwa na helikopta walikuwa wakijitahidi kuwaokoa watu waliokuwa katika bandari ya La Restinga, kwenye kisiwa cha El Hierro,” ilieleza taarifa hoyo.

Vyombo vya habari vya Uhispania vimeripoti kuwa takriban Wahamiaji 150 walikuwemo ndani ya boti hiyo na juhudi za kuwatafuta manusura bado zinaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *