SITA WADAKWA KWA MAUAJI YA ASKARI POLISI ARUSHA

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, limewakamata watu sita wanaotuhumiwa kwa mauwaji ya Askari Polisi, Roland Mollel, usiku wa Aprili 15 katika eneo la Mlimani, Kata ya Muriet.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea wakati askari huyo alipokuwa akifanya shughuli zake binafsi baada ya kazi.

“Kabla ya tukio hilo, kulizuka taharuki miongoni mwa wananchi kufuatia taarifa za kuwepo kwa watu waliodaiwa kuwa wezi katika eneo hilo,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Inadaiwa kuwa, katika mkanganyiko huo, marehemu akiwa amepanda pikipiki pamoja na mtu mwingine anayedaiwa kuwa dereva wa bodaboda, walishambuliwa na kundi la watu waliokuwa wakiwafukuza kwa tuhuma hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *