SIREMA WAANDAA KONGAMANO KUTAMBUA MCHANGO WA RAIS SAMIA SEKTA YA MADINI

Na Saulo Stephen – Singida.

Katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Madini, Chama cha wachimbaji Madini Mkoa wa Singida SIREMA kimeandaa kongamano la kupongeza na kutambua Mchango wa Rais katika Sekta hiyo.

Akiongea na Jambo Media kuelekea kongamano hilo, Mjumbe wa kamati tendaji ya SIREMA Mkoa wa Singida, Paschal David Nzuri amesema kongamano hilo la kumpongeza na kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan litafanyika Agosti 23 mwaka huu katika eneo la Machimbo ya Sekenke lililopo wilayani Iramba Mkoani Singida huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Madini Antony Mavunde.

Ameongeza kuwa lengo la kupeleka kongamano hilo katika eneo hilo ni kutokana na historia iliyopo katika Machimbo hayo hususani katika kipindi cha Ukoloni.

Kwa upande wake Bi.Martha Alex Kayaga ambaye ni Mwenyekiti na Mwakilishi wa Wanawake wa wachimbaji Madini kupitia Shirikisho la wanawake FEMATA amesema Wachimbaji Madini Mkoa wa Singida wamejipanga kumpongeza na Kumshukuru Raisi Simia kupitia kongomano hilo kutokana na maeneo waliyopatiwa wachimbaji madini pamoja na Leseni kwa wachimbaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *